HabariPilipili FmPilipili FM News

HELB Kusaidia Serikali Kulipa Deni

Wizara ya elimu kupitia bodi ya kutoa mikopo kwa elimu ya juu HELB sasa inataka waajiri wa kampuni na mashirika kusaidia serikali kulipa deni la shilingi bilioni 7.2 kutoka kwa wafanyakazi ambao walinufaika na fedha za HELB.

Waziri wa elimu Amina Mohamed amesema jumla ya wanafunzi  74,000 wangali wanadaiwa na serikali miaka mingi baada ya kukamilisha masomo yao.

Aidha Waziri Amina amesema ili kuafikia hili watashirikiana na idara ya sheria akisema  hii itasaidia wanafunzi wengine wenye uhitaji mkubwa wa fedha hizo.

Naye mwenyekiti wa kamati ya HELB Ekwe Ethuro ameelezea kuhusu umihimu wa kupigana na ufisadi katika mfuko wa hazina ya HELB akisema  iwapo hili likitaafikiwa litasidia pakubwa kuimarisha  fedha za HELB katika siku za usoni.

Walikuwa wakizungumza katika sherehe ya uzinduzi wa mpangilio wa HELB wa miaka mitano ijayo walikaohidi kuimarisha kiwango cha masomo ya juu kupitia mfuko wa HELB.

Show More

Related Articles