HabariMilele FmSwahili

Serikali kuwasaka waliokwepa kulipa mkopo wa HELB

Zaidi ya wanafunzi 70,000 wanasakwa na serikali kwa kukwepa kulipa mkopo wanaodaiwa na bodi ya ufadhili wa masomo ya juu nchini. Akizungumza katika warsha ya uzinduzi wa mikakati mipya ya bodi hiyo mapema leo, waziri wa elimu balozi Amina Mohammed ameapa kutowasaza wanafunzi hao mpaka watakapowajibikia deni hilo la kima cha takribani shilingi bilioni 7. Amina anasema hii ndiyo njia pekee itakayosaidia kutoa msaada kwa wanafunzi wanaonuia kujiunga na vyuo vikuu mwaka huu.

kauli iliyopigiwa upatu na mwenyekiti wa bodi hiyo ya mikopo Ekwe Ethuro

Hata hivyo kama mojawapo ya kuvikwamua vyuo anuwai ,serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 300 kwa wanafunzi watakaojiunga na vyuo hivyo mwaka huu

Show More

Related Articles