HabariMilele FmSwahili

IEBC yalalamikia mgao finyu wa bajeti

Tume ya uchaguzi IEBC nayo imelalamikia mgao finyu ambao kwa miaka kadhaa ya kifedha imekuwa ikipokea. Kaimu afisa mkuu mtendaji IEBC Marjan Hussein akifika mbele ya kamati ya bunge kuhusu haki anasema mwaka wa kifedha 2018/19 waliirtisha  shilingi bilioni 13 japo walipewa shilingi bilioni 4 fedha anazosema zinatosha mishahara ya wafanyakazi pekee. Anasema mwaka 2019/20   licha ya kuitisha shilingi bilioni 13.5 ni bilioni 4.7 walipewa. Anasema kutokana na mgao huo umekuwa vigumu kutekeleza mojawapo wa ajenda kuu zao ambayo ni kuhamisha makao makuu ya IEBC kutoka jumba la Aniversary hapa Nairobi. Anahofia huenda swala la ukaguzi mipaka likatatizika kwa uksoefu wa fedha

Show More

Related Articles