HabariMilele FmSwahili

Gavana wa Samburu Moses Lenolkula amulikwa na EACC kuhusu madai ya ufisadi

Tume ya EACC inasema itamshtaki gavana wa Samburu Moses Lenolkula na maafisa wengine wa kaunti hiyo akiwemo msaidizi wake na spika wa bunge hilo kwa tuhuma za ubadhirifu wa shilingi bilioni 2 fedha za umma. EACC katika taarifa inasema imepata ushahidi ambao utatawezesha kuwashtaki maafisa hao baada ya maafisa wake kuvamia na kukusanya maelezo katika makaazi ya Lenolkula mtaani Karen pamoja na afisini mwake, msako mwingine ulioendeshwa katika makaasi ya msaidizi wake  Simon  Etiene, makaazi ya spika wa bunge la Samburu Solomon Lempere na maafisa wengine wa kaunti. EACC inasema maafisa hao wameweza kujinufai na fedha hizo katika muda wa miaka 4 iliyopita. Katika barua iliyotiwa saini na afia mkuu mtendaji wa EACC Twalib  Mbarak, inasema baadhi ya maafisa wa kaunti walijipatia tenda za serikali zilizogharimu shilingi milioni 700. Shilingi zingine bilioni 1 nazo zinaarifiwa kukabidhiwa baadhi ya wanakandarasi ambao licha ya malipo hayo hakuna kazi wametekeleza kaunti hiyo. Twalib anasema mchakato wa kurejesha fedha hizo umeanza kwa kufungwa akaunti za wauhusika sawa a kutwaliwa mali zao. Kaunti ya Samburu ni miongoni 8 mwa zilizotajwa na bunge la seneti kufeli kuelezea kuhusu zilivyotumia fedha za umma.

Show More

Related Articles