HabariPilipili FmPilipili FM News

Walioharibu Tunnel Ya Dongo Kundu Kugharamika Kuikarabati Yasema KENHA.

Maafisa wa halmashauri ya ujenzi wa barabara kuu KENHA sasa wanasema mmiliki wa lori lililosababisha ajali katika barabara mpya ya Dongo Kundu by pass atalazimika kugharamikia hasara aliyosababisha dereva wa lori hilo.

Kulingana na mmoja wa maafisa hao wa KENHA dereva wa lori hilo alikuwa akiendesha kwa kasi na kusababisha ajali hiyo ikiwemo hasara ya shilingi milioni 10.

Wakati huo huo amesema ukarabati wa barabara hiyo ya dongu kundu utafanywa kwa haraka ikizingatiwa kwamba inasaidia pakubwa katika shughuli za kupaa na kutua kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Moi.

Dereva huyo kwa sasa anaendelea kupokea matibabu hospitalini huku wito ukihimizwa kwa madereva kuwa makini zaidi.

Show More

Related Articles