HabariPilipili FmPilipili FM News

Achoki Ataoa Makataa Kwa Wazazi Mombasa.

Kamishna wa kaunti ya mombasa Evans Achoki amewataka wazazi na wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la nane mwaka jana ambao hawajajiunga na kidato cha kwanza kufika mara moja katika shule za msingi walizosomea ili serikali itambue tatizo linalowakumba.

Achoki anasema wazazi wanaoendelea kuwaficha watoto wao watachukuliwa hatua kali ya kisheria  huku akisema tayari makataa ya serikali yamekwisha hivyo kwanzia juma lijalo mzazi ambaye atakuwa hajafuata sheria hiyo atachukuliwa hatua kali ya kisheria.

Aidha achoki amewataka wazazi ambao wanaugumu wa kuwapeleka watoto wao katika shule za mbali kuwataftia shule za karibu watoto wao akisema shule nyingi za upili eneo la pwani bado ziko na nafasi.

Show More

Related Articles