HabariPilipili FmPilipili FM News

Polisi Wanachunguza Mauaji Ya Wakili Robert Chesung.

Maafisa wa polisi wanachunguza video iliyonaswa na kamera za siri zikionyesha jinsi washukiwa wawili walimuua wakili wa mahakama ya juu, Robert Chesung akiwa nyumbani mwake Lukenya, katika kaunti ya Machakos.

Kulingana na video hiyo, washukiwa hao walimlazimisha mlinda lango kuwaelekeza kwa nyumba ya Chesung.

Baada ya wao kubisha mlango Chesung anaonekana kuchungulia kwenye pazia la dirisha lake, ambapo mmoja wa washukiwa hao alimpiga risasi mara 3 kifuani na kumuua.  Kulingana na afisa mmoja wa polisi, Chesung aliishi akihofia maisha yake.

Aidha, chama cha mawakili nchini (LSK) wakiongozwa na rais wao Allan Gichuhi, wamekashifu vikali mauaji hayo huku wakimtaka inspekta generali wa polisi, Joseph Boinnet kuingilia kati ili kuhakikisha haki imetendeka.

Show More

Related Articles