HabariMilele FmSwahili

Jamaa aliyeshtakiwa kwa jaribio la kukwepa KNH bila kulipa ada za matibabu ya mwanawe aachiliwa huru

Jamaa wa miaka 22 aliyeshtakiwa kwa jaribio la kukwepa hospitali ya kitaifa ya Kenyatta bila kulipa ada za matibabu ya mwanawe wa mwaka mmoja amejumuika na familia yake alasiri hii. Bonface Murage aliachiliwa mapema leo baada ya muingilio wa gavana Mike Sonko aliyelipa bili ya shilingi elfu 56 alokuwa akidaiwa katika hospitali hiyo. Akizngumza nje ya mahakamani ya Milimani baada ya kupata uhuru wake, Murage hakusita kuonyesha furaha yake akionekana pia kujutia kitendo hicho, ila akasema ukosefu wa fedha ulipelekea masaibu yake.

Murage mkaazi wa Rongai sasa atakuwa chini ya uangalizi wa maafisa wa mahakama kwa mieiz mitatu ijayoo.

Katika hali ya kumpiga jeki zaidi, gavana Mike Sonko ameahidi kumsaidia kupata ajira ili aweze kujikimu pamoja na familia yake.

Show More

Related Articles