HabariPilipili FmPilipili FM News

Mahakama Yamwachilia Huru Jamaa Aliyejaribu Kumtorosha Mwanawe Hospitali.

Mwanamume aliyejaribu kumtorosha mwanawe kutoka hospitaini kwa sababu hakua na fedha za kugharamia matibabu yake, ameachiliwa huru na mahakama.

Mahakama imesema kuwa yuko huru lakini atatakiwa kutojihusisha na uhalifu wa iana yoyote kwa muda wa miezi mitatu ijayo.

Jamaa huyo kwa jina Bonface Murage ameeleza furaha yake akisema hakuwa na budi ila kumuiba mwanamwe huyo kufuatia ukosefu was hilingi elfu 56 bili ya hospitalini.

Yakijiri hayo wahisani wamejitolea kulipa bili hiyo ya hospitali huku wengine wakimpatia jamaa huyo fedha za kujikimu kwa muda.

Show More

Related Articles