HabariMilele FmSwahili

Mgomo wa wauguzi waingia wiki ya tatu

Huduma za matibabu zimeendelea kuathirika hospitali tofauti za umma wauguzi wakiendeleza na mgomo wao kwa wiki ya tatu sasa.Kaunti za Bomet na Kakamega ni za punde kwa wauguzi kujiunga na wenzao kutoka kaunti 19 wanoendelea na mgomo huo.Huko Kakamega wagonwja wamelalamika kukosa huduma tangu majira ya asubuhi wakitaka usimamizi wa kaunti kuangazia lalama za wauguiz kuwawezesha kurejea kazini.

Hali sawia imeshuhudiwa kaunti ya Bomet, ambako wauguzi wakiongozwa na naibu katibu Bernard Langat wanasema hawako tayair kutii agizo la rais iwapo hakuna utekelezwaji wa mkataba waliosaini na serikali za kaunti.

Hayo yanajiri wakati serikali ikiendelea kutaka wauguzi wanaogoma kushtakiwa kwa kukaidi agizo la mahakama ililoharamisha mgomo wao.Katika mahakama ya Leba, mawakili wa sirikali wanahoji kwmaba kwa wauguzi kuendelea kushiriki mgomo huo ni dharau sio tu kwa mahakama bali pia wakenya ambao wanataraji huduma kutoka kwao.

Hata hivyo wauguiz wanasisitiza hawajapokea amri yoyote ya mahakama kusitisha mgomo, kwani mgomo huio ulitangazwa kaunti mbalimbali.

Show More

Related Articles