HabariMilele FmSwahili

Usajili wa wakenya kupitia mfumo wa NIIMS kufanyiwa majaribio katika kaunti 15 kuanzia leo

Usajili wa wakenya na raia wa kigeni kupitia mfumo mpya wa usimamizi na usajili wa taifa unatarajiwa kufanyiwa majaribio kuanzia leo. Zoezi hilo litaendeshwa kaunti 15 kabla ya shughuli rasmi kuanza mwezi Machi. Katibu katika wizara ya sualama wa taifa dkt Karanja Kibicho anasema katika zoezi hili taarifa zote zitanakiliwa kwa utumiaji wa vifaa vitaka vyochukua alama ya vidole na utambulisho wa uso, mbali na majina, uraia, elimu, taarifa za wazazi, nambair ya utambulisho maarufu pin, nambari za NHIF na NSSF miongoni mwa taarifa zingine mpya. Mradi huu ambao utagharimu serikali takriban shilingi bilioni 6 unanuia kuhakikisha kila mkenya anapewa kadi ya huduma kuanzia watoto wa miaka 6 hadi wakongwe.

Kaunti hizo ni pamoja na Nairobi, Baringo, Uasingishu, Marsabit, Embu, Makueni, Kisumu, Kisii, Wajir, Tanariver, Busia, Kajiado, Kilifi, Nyandarua na Kiambu.

Haya yanajiri wakati tume ya haki za binadamu ikitilia shaka zoezi hilo. KHRC inasema kuan baadhi ya masuala ambayo yanapaswa kutathminiwa kabla ya kuendeshwa. KHRC inasema hakuna hakikisho kuwa taarifa za wakenya zitalindwa.

Show More

Related Articles