HabariPilipili FmPilipili FM News

Wizara Ya Leba Kukutana Na Washikadau Wa Afya Jumamosi.

Wizara ya leba sasa inapanga kufanya  mkutano na washikadau katika sekta ya afya jumamosi hapo kesho  ili kujadili mgogoro uliopo kuhusu mgomo wa wauguzi.

Waziri wa Leba Ukur Yattani, anasema mkutano huo unalenga kutafuta njia ya kuleta upatanisho kama ilivyoagizwa na mahakama ya leba, ambayo awali iliagiza wauguzi kusitisha mgomo kwa siku 60,  ili kupisha mazungumzo.

Kuhusu wauguzi waliokaidi amri ya rais ya kuwataka kurejea kazini leo, Yatani amesema hatma yao iko mikononi mwa serikali za kaunti husika, akishikilia kuwa mgomo wao ni haramu.

 

Show More

Related Articles