HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwanafunzi Wa Darasa La Tatu Ajitia Kitanzi Kilifi.

Polisi wanachunguza kisa ambapo mwanafunzi mmoja mwenye umri wa miaka 13 amepatikana akiwa amefariki kaunti ya Kilifi.

Mwanafunzi huyo wa darasa la tatu kutoka shule ya msingi ya ADC huko Magarini, anadaiwa kujitia kitanzi katika kijiji cha Mtangani MAJIVUNI.

Kufikia sasa sababu ya yeye kujitoa uhai bado haijabainika.

RACHEAL MALINGI aliye naibu chifu wa eneo hilo anasema  Jackson Changawa alitoka nyumbani akirudi shuleni baada ya kula chakula cha mchana, kabla ya mwili wake kupatikana ukining’inia juu ya mti saa chache badae.

Mkuu wa polisi eneo hilo Gerald Barasa amesema tayari uchunguzi umeanzishwa.

Show More

Related Articles