HabariPilipili FmPilipili FM News

Atwoli Amtaka Waziri Wa Leba Ajiuzulu.

Katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli sasa anamtaka waziri wa leba Ukur Yattani kujiuzulu.

Atwoli anasema baraza la magavana na waziri Yattani walimpotosha rais Uhuru Kenyatta kuhusu mgomo wa wauguzi, ilihali ni jukumu lao kuketi na wadau husika ikiwemo wakuu wa wauguzi , kuutafutia ufumbuzi mgogoro uliopo.

Yakijiri hayo Baraza la magavana limewaonya vikali wauguzi watakaokaidi amri ya rais kuwataka kurejea kazini kufikia saa mbili asubuhi hii leo.

Show More

Related Articles