HabariPilipili FmPilipili FM News

Onyo La Baraza La Magavana Kwa Wauguzi.

Baraza la magavana limewaonya vikali wauguzi watakaokaidi amri ya rais kuwataka kurejea kazini kufikia saa mbili asubuhi hii leo.

Mwenyekiti wa baraza hilo gavana wa kakamega Wyclif Oparanya anasema madai ya wauguzi kwamba hawajapokea maagizo ya mahakama kuwataka kusitisha mgomo ni uongo.

Kauli yake imeungwa mkono na waziri wa afya Sicily Kariuki akisema serikali imejitolea kuangazia malalamishi ya wauguzi, kupitia vikao ambavyo vinaandaliwa na kamati iliyoteuliwa na wizara ya leba.

Show More

Related Articles