HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwatha Alifariki Kutokana Nakuvuja Damu Nyingi Asema Mwanapatholojia.

Imebainika kuwa mwanaharakati Caroline Mwatha alifariki kutokana na kuvuja damu wakati akiavya mimba.

Hayo yamethibitishwa na mwanapatholojia wa serikali Joharnes Oduor pamoja na wa  jamaa za familia yake, walioongoza zoezi la upasuaji wa mwili wake huko Nairobi hapo jana.

Matokeo ya upasuaji huo pia yamebaini kuwa nyumba ya uzazi ilikua na majeraha mabaya hali iliyosababisha marehemu Mwatha kuvuja damu nyingi. Aidha Kijusi chake pia kilikua na majeraha mabaya.

Wanapatholojia hao hata hivyo wametaka polisi kukamilisha uchunguzi wao kubaini iwapo uaviaji mimba ulifanywa kwa hiari ya Mwatha au la.

Kufikia sasa watu 8 wanazuiliwa na polisi akiwemo dakitari wa kituo cha afya cha new njiru community center huko dandora Nairobi, ili kusaidia polisi na uchunguzi kuhusu kifo cha mwanaharakati huyo.

Show More

Related Articles