HabariPilipili FmPilipili FM News

Spika Ruwa Apinga Madai Ya Ufisadi Dhidi Yake.

Spika wa bunge la Kwale  Sammy Ruwa  amekanusha madai  yanayoibuliwa na wawakilishi wadi katika bunge hilo kwamba anahusika na ufisadi ,utumizi mbaya ya mamlaka na uchochezi wa kikabila akiyataja matamshi hayo kulenga kumharibia jina .

Ruwa amesema tofauti zinazoibuka bungeni humo ni kutokana  na baadhi ya wajumbe kupinga azma yake  ya kutaka kiti cha ugavana ujapo uchaguzi mkuu mwaka 2022. Hata hivyo anasema hakuna kitakacho mzuia kuwania wadhfa huo .

Spika huyo wa bunge la kaunti ya kwale amewataka wanaomtuhumu kuhusika na ufisadi kumchukulia hatua za kisheria endapo  wako na ushaidi  wa kutosha  kwamba alishirikiana na karani wa bunge Dennis Mutui kufuja fedha za umma.

Show More

Related Articles