HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwili Wa Mwatha Kufanyiwa Upasuaji Kubaini Ukweli Kuhusu Kifo Chake.

Mwili wa mwanaharakati Caroline Mwatha unatarajiwa kufanyiwa upasuaji hii leo kubainisha kilicho sababisha kifo chake.

Naibu kamanda wa polisi kaunti ya Nairobi Richard Kerich amesema upasuaji wa mwili huo utafanywa katika chumba cha maiti cha CITY,ambapo mwili wake umekuwa ukihifadhiwa kwa zaidi ya wiki moja.

Taarifa za polisi zinadai Mwatha alifariki akijaribu kuavya mimba katika kituo cha afya huko dandora kaunti ya Nairobi. FAMILIA yake imeyapuuzilia mbali madai hayo, Babake Stanslous Mbai akidai mwanawe hakuwa mja mzito, na hata angekuwa mja mzito hangeitoa mimba hiyo.

Yakijiri hayo jamaa anayedaiwa kuwa mpenzi wake Mwatha Alexander Gikonyo , ni miongoni mwa washukiwa 6 wanaozuiliwa na polisi kwa kuhusishwa na kifo cha mwanaharakati huyo. AIDHA  Joshua Ochieng mumewe marehemu na ambaye alikuwa dubai wakati wa tukio hilo, ametaka uchunguzi wa kina kufanywa na wahusika kuchukuliwa hatua .

Show More

Related Articles