HabariPilipili FmPilipili FM News

Kauli Ya Owen Baya Kuhusu Mstakabali Wa Uongozi Pwani.

Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya sasa anawataka viongozi wote wa kisiasa Pwani wenye ari ya kuongoza mwelekeo wa siasa za wamijikenda  kuanza mchakato unaolenga kudhibiti siasa za eneo hili bila kutegemea uongozi wa chama cha ODM.

Akizungumza  mjini Kilifi Baya anasema licha ya wakaazi wengi eneo la Pwani kwa muda mrefu wamekuwa wakiunga mkono chama hicho,baadhi ya viongozi wa chama hicho eneo hili wanaendelea kupoteza nyadhifa zao hatua ambayo ameitaja kama ishara tosha  ya kusambaratika kwa siasa ya wamijikenda ndani ya chama hicho.

Kauli yake inajiri siku chache tu baada ya chama cha Umoja Summit Party kuzinduliwa huku kikitajwa kuwa mojawapo ya chama kinacholenga kutoa mwelekeoa wa kisiasa pwani.

Show More

Related Articles