HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Kilifi Kukosa Maji Baada Ya Nguvu Za Umeme Kukatwa Baricho.

Wakaazi  wa kaunti ya Kilifi  watalazimika kukosa huduma za maji  kutokana  na kukatwa  kwa nguvu za umeme  huko  baricho kwenye  kaunti hiyo.

Kiringi Mwachitu ambaye ni waziri wa maji katika kaunti hiyo anasema hali hiyo imechangiwa na deni kubwa la umeme la shilingi milioni 7 unusu, zinazodaiwa kampuni 3 za maji ikiwemo , malindi water, kilifi water pamoja na mombasa water.

Hata hivyo anasema serekali ya kaunti hiyo imefanya mazungumzo na wadau husika ili kuweka mikakati itakayotoa suluhu mwafaka.

Show More

Related Articles