HabariMilele FmSwahili

Licha ya agizo la Rais wauguzi waapa kutorejea kazini

Mgomo ungalipo, ni kauli ya wauguzi ambao wanagoma katika kaunti mbalimbali licha ya agizo la rais kuwataka kurejea kazini kufikia Ijumaa.Katibu mkuu wa wauguzi akitoa taarifa kuhusiana na mgomo huo anasema wanaamini mgomo wao umelindwa kisheria na walifuata taratibu zote kabla ya kuuitisha.

Panyako anasisitiza kaunti ambazo zimetii maafikiano yao ya Novemba mwaka 2017 ikiwemo Migori, Machakos, Kwale, Nairobi, Mombasa na Vihiga wauguzi tayari wamerejelea shughuli.

Show More

Related Articles