HabariMilele FmSwahili

Rais awaagiza wauguzi wanaogoma kurejea kazini

Wauguzi wote wanaogoma sharti warejee kazini Ijumaa hii saa mbioli asubuhi. Ni agizo la rais Uhuru Kenyatta ambaye pia amewaagiza polisi kuwakabili vikali wauguzi wanaonuia kuwahujumu wenzao walio kazini. Rais ameiagiza wizara ya afya na serikali za kaunti kuwafuta kazi na kuwachukulia hatua za kisheria wauguzi watakaokaidi agizo la kurejea kazini.

Akizungumza baada ya kukutana na wakuu wa baraza la magavana rais ametaja mgomo unaoendelea kuwa haramu hasaa baada ya mahakama ya leba kuagiza mgomo wao kusitishwa kwa siku 6o ili kuruhusu mazungumzo ya upatanisho na serikali.

Show More

Related Articles