HabariMilele FmSwahili

Mwili wa mwanaharakati Caroline Mwatha kufanyiwa upasuaji leo

Mwili  wa mwanaharakati Caroline Mwatha unatarajiwa kufanyiwa upasuaji leo kubaini chanzo cha kifo chake. Awali polisi katika taarifa walisema kuwa marehemu alifariki baada ya jaribio la kuavya mimba ya miezi 5 katika kilini moja mtaani Dandora. Aidha mmiliki na mtu anayedai kuwa daktari wa kliniki ambako marehemu aliripotiwa kuavya mimba wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo. Hii ni baada ya mmiliki wa kliniki hiyo kukiri kuwa walipeleka mwili wake katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City na kumwandikisha kwa jina tofauti na maelezo kuwa alifariki kutokana na ugonjwa wa kuendesha. Idara ya DCI imedhibitisha kuwa inawahoji watu 6 kuhusiana na tukio hilo. Familia ya Caroline na wanaharakati nchini wameitisha uchuguzi huru kuhusiana na kifo chake.

Show More

Related Articles