Swahili Videos

Vifo vya watoto hospitali ya Kiambu

Hospitali ya kaunti ya Kiambu iko kwenye mizani ikichunguzwa kuhusiana na vifo vya zaidi ya watoto wachanga watano waliofariki kwenye kiangulio kati ya alhamisi na hiyo jana,  katika hali tatanishi.
Wazazi hao wanadai kuwa huenda mashine hizo hazifanyi kazi na zinatumiwa na  wauguzi wanagenzi na kusababisha vifo vya wanatoto hao wachanga.
Hata hivyo, msimamizi wa hospitali hiyo amekanusha vikali madai madai hayo licha ya kukiri kwamba watoto 20 wachanga walifariki hospitalini humo mwezi jana pekee.

Show More

Related Articles