HabariPilipili FmPilipili FM News

Spika Wa Bunge La Kwale Ajipata Pabaya.

Kizaazaa kimeshuhudiwa  katika bunge la Kwale  baada ya wawakilishi wadi waliofika bungeni humo  kumzuia  spika  sammy ruwa  kufungua  rasmi vikao vya bunge hilo baada mabunge yote nchini kufunguliwa rasmi hii leo baada ya likizo ya Krismasi.

Wawakilishi hao waliojawa na ghadhabu  wamefunga  mlango wa bunge   na kumzuia spika Ruwa kuingia  wakidai kwamba anakumbwa  na  kashfa za ufujaji wa fedha ,utumizi mbaya wa  mamlaka  na uchochezi wa kikabila  unaosababisha migongano ndani ya bunge hilo.

Kiongozi wa waliowengi  katika bunge la kwale aliyepia mwakilishi wadi ya Ramisi Raia Mkungu amemtaja spika Ruwa kama kiongozi aliyekosa maadili na anatekeleza kazi zake kinyume na sheria  hatua inayosambaratisha shughuli za bunge hilo pamoja na kuwakandamiza wawakilishi wadi.

Aidha wamemshtum vikali spika huyo kwa kuchangia pakubwa kufurushwa  afisini  kwa karani wa bunge hilo Dennis Mutui kwa madai ya ufisadi  swala wanalosema spika wa bunge hilo alihusika katika ufujaji wa wake.

Show More

Related Articles