HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Junda Wakadiria Hasara Baada Ya Moto Kuteketeza Nyumba .

Takriban familia 12 zimelazimika kukesha nje kwenye baridi baada ya moto kuteketeza nyumba moja eneo la Junda mshomoroni hapa mombasa usiku wa kuamkia leo.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi eneo la Kisauni Christopher Limo amesema moto huo unaaminika kuzuka kutoka chumba kimoja cha nyumba hiyo yenye vyumba 12 ,mwendo wa saa mbili na nusu usiku baada ya Stove ya kupikia kulipuka.

Limo amesema hakuna aliyejeruhiwa wakati wa mkasa huo. Hata hivyo amewataka wenyeji kusalia wangalifu zaidi hasa katika masuala ya stima akiongeza kuwa tayari wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha mkasa huo.

Show More

Related Articles