HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Yalaumiwa Kwa Kutojenga Shule Zakutosha Pwani.

Viongozi wa pwani wanailumu serikali kwa kutojenga shule za kutosha pamoja na kutosambaza vifaa vya masomo, wakitaja hilo kuwa chanzo cha matokeo duni kwa wanafunzi.

Naibu wa gavana wa kaunti ya Mombasa Wiliam Kingi amesema wanafunzi wanaowacha shule na kujihususha na uendeshaji wa bodaboda ndio wa kwanza kupachika wanafunzi wa shule mimba.

Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo na mbunge wa Mvita Abdul Swamad Nassir kwa upande wao  wamesema maeneo bunge ya pwani yanajulikana kwa idadi ndogo ya shule licha ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi.

Show More

Related Articles