HabariPilipili FmPilipili FM News

Bunge Kurejelea Vikao Vyake Leo.

Wabunge wanatarajiwa kurejelea vikao vyake leo alasiri huku ikiwa tayari wabunge wameainisha baadhi ya mambo yatakayo pewa kipao mbele.

Kati ya masuala ibuka ni pomoja na kupasishwa bajeti ya ziada , kwamuliwa tarehe ya kujadili mswada wa usawa wa kijinsia wa thuluthi mbili, pamoja na  mapendekezo ya kuifanyia marekebisho tume ya uchaguzi nchini.

Mengine ni pamoja na masuala ya zoezi la  hesabu ya watu linalopangwa kufanyika badae mwaka huu, kama wanavyosimulia kiongozi wa wqengi bungeni Aden Duale na mwenzake wa wachache John Mbadi.

Kamati nyengine za bunge kama vile kamati ya haki na masuala ya haki na sheria inayoongozwa na mwenyekiti wake William Cheptumo pia inatazamiwa kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kuifanyia marekebisho katiba pamoja na mageuzi yanayopaswa kufanywa kwa tume ya uchaguzi nchini IEBC.

Show More

Related Articles