HabariMilele FmSwahili

IEBC kuweka wazi ripoti yake kuhusiana na uchaguzi mkuu wa 2017

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC leo itaweka wazi ripoti yake kuhusiana na uchaguzi wa tarehe nane mwaka wa 2017 na marudio ya uchaguzi wa urais mwezi Okotba mwaka huo.Ripoti hii inatarajiwa kuangazia masuala tofauti kuhusiana na zoezi zima la uchaguzi, changamoto ilizokabiliwa nayo na mapendekezo ambayo IEBC inanuia yaangaziwa kufanikisha zaidi chaguzi zijazo. Ripoti hii ni muhimu katika mkakait wa IEBC kuendesha chaguzi huru na haki siku za mbeleni. Inatolewa wakati kukiwa na tuhma mbalimbali kwa IEBC kuhusiana na jinis ambavyo iliendesha uchaguzi huo, baadhi ya wanasiasa wakiilaumu wakati wenginie wakiipongeza kwa kuendesha uchaguzi wa kuridhisha.

Show More

Related Articles