HabariMilele FmSwahili

Wafanyikazi kaunti ya Nairobi watishia kugoma Leo

Wafanyakazi kaunti ya Nairobi wameitisha mgomo wao kuanzia leo kutokana na kile wanachokitaja kama kukosa kutekelezwa mkataba wao wa makubaliano na gavana Nairobi Mike Sonko wa  mwaka wa 2012. Gavana Sonko aliahidi  kutelekeza mkataba huo mwezi Januari mwaka huu lakini hilo halijatimizwa hadi sasa. Zaidi ya wafanyakazi 13,000 wanatarajiwa kukongamana nje ya afisi za kaunti asubuhi hii kushinikiza kuheshimiwa haki yao. Wafanayakazi hao wanadai nyongeza ya mshahara kwa kati ya asilimia 15 hadi 28. Mkataba huo una makubaliano aina mbili yaani monetary na non-monetary ambao utawaruhusu wafanyakazi kufaidi katika likizona bima ya hospitali miongoni mwa mambo mengine.

Show More

Related Articles