HabariMilele FmSwahili

Huduma za matibabu kusambaratika zaidi mgomo wa wauguzi ukiingia wiki ya pili

Huduma za matibabu zitasambaratishwa zaidi katika hosipitali za umma nchini kuanzia leo baada ya wauguzi katika kaunti 3 kujiunga na wenzao kutoka kaunti 10 kwenye mgomo huo. Aidha wauguzi katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta hapa Nairobi wanartarajiwa kujiunga na wenzao kwenye mgomo huu. Mgomo huu unaingia wiki ya pili jiithada zaidi pia zikitarajiwa kutekelezwa na kamati maalum aliyobuni waziri wa leba Ukur Yattani kuangazia mgomo huo.Ni mgomo unaowadia huku maafisa wa kliniki pia wakitishia kugoma kulalamikia kutoangaziwa maslahi yao. George Gibore, katibu mkuu wa muungano wa maafisa wa kliniki anasema iwapo hawatapewa walioafikiana hawako tayari kurejea mazungumzo ila kuenlekea mgomo.

Show More

Related Articles