HabariMilele FmSwahili

Makamanda wapya wakamilisha mafunzo kuhusu uongozi

Makamanda wapya walioteuliwa maajuzi wamekamilisha mafunzo kuhusu uongozi. Makamanda hao walioteulwia na inspekta generali wa polisi sasa wanajiandaa kuanza kutekeleza majukumu yao rasmi ikiwemo jukumu mpya aliowapa rais kusimamia mikutano ya kiusalama na maendeleo maeneo yao. Akiwazungumzia baada ya kukamilisha mafunzo hayo inspekta genereali wa polisi Joseph Boinnet anasisitiza watahitajika kuwajibikia utendakazi wao, akiwaonya watabeba msalaba patakapotokea changamoto zozote.

Waziri wa usalama wa taifa dkt Fred Matiangi awali aliwaagiza makamanda hao kushirikiana na maafisa wengini wa usalama kuweka mikakait ya kutosha ya kudumisha usalama.

Show More

Related Articles