HabariMilele FmSwahili

Usalama waimarishwa katika chuo kikuu cha JKUAT Juja, wanafunzi wakitishia kuandamana

Maafisa wa polisi wameimarisha doria nje ya chuo kikuu cha Jomo Kenyatta Juja kaunti ya Thika maandamano wa wanafunzi yakinukia. Wanafunzi hao wamedokeza nia ya kuandaa maandamano kulalamikia kile wanadai ni kukithiri mauaji ya kiholela ya wenzao. Ni kufuatia kisa ambapo mwanafunzi wa kike alidaiwa kudungwa kisu na majambazi karibu na hoteli moja eneo hilo usiku wa kuamkia jana.

Show More

Related Articles