HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakulima 200 Waidai Kampuni Ya KISCOL Milioni 8

Zaidi ya wakulima 200 wa miwa kaunti ya Kwale wanautaka  usimamizi wa kampuni ya  kiwanda cha uzalishaji sukari  cha kiscol huko Ramisi kuwalipa deni lao la jumla ya shilingi  milioni 8 wanazodai kiwanda hicho baada ya kuwauzia miwa  mwaka uliopita.

Wakulima  hao  waliokuwa wakizungumza  na wanahabari huko Eshu eneo bunge  la Lungalunga  wanasema tangu serikali  kukifunga  kiwanda cha Kiscol mwaka uliopita kwa madai  kwamba  wanaendeleza biashara ya sukari gushi usimamizi wa kiwanda hicho pia ulisitisha malipo kwa wakulima hao kwa madai kwamba biashara  ya uuzaji sukari ilidumazwa  na serikali.

Hata hivyo afisaa wa mawasiliano  katika kiwanda hicho cha Kiscol  Mathius Mutua ameyakanusha  madai hayo akisema kwamba  hakuna mkulima anayedai pesa yoyote kutoka kwa usimamizi wa kiwanda hicho.

Show More

Related Articles