HabariPilipili FmPilipili FM News

Wananchi Wa Matuga Walilia Mradi Wa Dongo Kundu.

Wakaazi wa Matuga Kwale wanalalamikia ukosefu wa ajira ndogondogo  katika mradi wa ujenzi ya barabara ya Dongokundu by pass unaoendelezwa kwa sasa katika awamu ya pili, wamkitaka  mbunge wa eneo hilo Kassim Sawa Tandaza kuingilia kati swala hilo ili kuona kwamba wanafaidika  na  ajira katika mradi huo.

Wanasema mradi huo bado haujamfaidi mkaazi yeyote wa Matuga katika maswala ya ajira ndogondogo licha ya kwamba barabara hio inaunganisha kaunti hio ya kwale na ile ya Mombasa.

Hata hivyo mbunge wa Matuga Kassim Sawa Tandaza ameahidi kulifuatilia swala hilo ili kuona kwamba dhulma hizo zinakomeshwa huku akitoa changamoto kwa vijana  kutafuta ajira zilizo na msingi badala ya kung’ang’ania vibarua vya raha leo.

Show More

Related Articles