HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Mombasa Walalamikia Idara Ya Uhamiaji Kuchelewesha Kutoa Stakabadhi za Usafiri (Pasipoti)

Wananchi kaunti ya Mombasa wamelalamikia kucheleweshwa kwa paspoti zao katika afisi za idara ya uhamiaji, wakisema wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu bila kupata stakabadhi zao.

Baadhi yao sasa wanasema wamelazimika kuahirisha safari zao za wiki ijayo, kutokana na hali hiyo.

Wanaitaka serikali ya kitaifa kupitia idara ya uhamiaji kuweka mikakati kabambe kuona kuwa wasafiri wanapata paspoti zao kwa wakati.

Juhudi zetu kuwataka maafisa wa idara hiyo kaunti ya Mombasa kuweka wazi hali ilioko, hazikufaulu baada ya wao kudinda kuzungumzia suala hilo.

Show More

Related Articles