Swahili Videos

Ukoko wa Jamii : Mila inayokataza wanawake kula firigisi

Wanasema mluhya na kuku ni sawia na mjaluo na samaki yaani ni kumaanisha kuwa kuku ndiyo kitoweo asili cha jamii ya waluhya.
Je wajua kuwa jamii hiyo ina masharti ya kupeana, kuchinja na kupakua sehemu za kuku na katika vipande vya kuku kuna sehemu maalum ya firigisi al-maaarufu “ Imondo” ambayo kamwe haifai kuliwa na wanawake, na wanaokula kisiri basi kamwe hawawezi kudumu katika ndoa.
Na kama anavyotuarifu baraka karama kwenye makala ya ukoko wa jamii, wazee wa jamii hiyo sasa wanasema asilimia kubwa ya wanawake ambao hawako katika ndoa huenda walikiuka sheria na kula “ imondo”.

Show More

Related Articles