HabariMilele FmSwahili

Wakili Khawar Qureshi aidhinishwa kushughulikia kesi ya ufisadi dhidi ya naibu jaji mkuu Philomena Mwilu

Wakili Khawar Qureshi atamwakilisha mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajji katika kesi ya ufisadi inayomkabili naibu jaji mkuu Philomena Mwilu. Aidha,maseneta James Orengo na Okong’o Omogeni wataendelea kumwakilisha mwilu kama mawakili wake kwenye kesi hiyo. Majaji watano wa mahakama kuu Hellen Omondi, Mumbi Ngugi, Francis Tuiyot,William Musyoka na Chacha Mwita wameamua kwamba Noordin alifuata taratibu hitajika kumteua Quresh kushiriki katika kesi hiyo.

Majaji hao aidha wamesema Noordin hakuwasilisha ushahidi kudhibitisha Orengo na Omogeni watatumia nyadhfa zao kuwa wanachama wa kamati ya sheria katika bunge la seneti kuwa na ushawishi katika kesi hiyo.

Mwilu alitaka Quresh raia wa Uingereza kuzuiwa kushiriki kesi hiyo kwa kigezo Noordin hakufuata sheria kumteua.Naye Noordin alitaka Orengo na Omogeni kufungiwa kwa kigezo ni maseneta na wanachama wa kamati ya sheria katika seneti ambayo hufuatilia shuguli za afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma.

Show More

Related Articles