HabariMilele FmSwahili

KNUT yajiunga na muungano wa COTU

Chama cha walimu KNUT imetangaza kujiunga upya na muungano wa wafanyikazi nchini COTU. Akitangaza hili katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion amewahakikishia walimu kuwa hatua hiyo itawezesha kuheshimiwa na kulindwa haki zao. Pia amesema hatua hiyo itaimarisha muungano na ushirikiano wa karibu baina ya wafanyikazi wote katika kutetea masakahi yao.

Naye katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli ametoa hakikisho kuwa COTU hautaingilia au kushawishi utendakazi wa KNUT. Ametoa hakikisho kuwa miungano wa wafanyikazi nchini itakuwa mdau muhimu katika masuala ya uongozi wa kitaifa.

Show More

Related Articles