HabariMilele FmSwahili

NTSA kuzindua leseni mpya za madereva za kidijitali leo

Mamlaka ya usalama barabarani NTSA itaanza leo kuwapa madereva lesini mpya za kidijitali. Katika taarifa NTSA imewataka wanaomiliki leseni za kale kuwasilisha taarifa zao kupitia mfumo wa kiteknolojia wa  TIMSI ili kuweza leseni mpya za  kidijitali. Leseni hizo  mpya zilifanyiwa majaribio mwezi Machi mwaka jana, na madereva watalipia shilingi elfu tatu kwa matumizi ya miaka 3. Kati ya mengine leseni hizi zitaweza kunasa na kunaliki makosa ya madereva na watakaogundulika kuhusika katika visa zaidi ya 40 vya utovu wa nidhamu bara barani watapokonywa lesini hiyo.

Show More

Related Articles