HabariMilele FmSwahili

Mbunge Ben Washiali ataka mpango wa kuwapa silaha walinzi wa kibinafsi kusitishwa

Kiranja wa wengi bungeni Ben Washiali anataka mpango wa kuwapa silaha walinzi wa kibinafsi kusitishwa hadi bunge lipasishe sheria kuweka taratibu za kutolewa silaha hizo.Washiali anasema iwapo silaha hizo zitatolewa bila sheria hitajika,huenda taifa likawa na silaha nyingi mikononi mwa raia ambazo zinaweza kutumika vibaya. Miongoni mwa mapendekezo yake ni kuhakikisha walinzi wote wa kibinafsi wanapata mafunzo maalum na kitengo cha kutoa leseni kufanyiwa mabadiliko.

Show More

Related Articles