HabariMilele FmSwahili

Ibada ya wafu ya wafanyikazi 6 wa hoteli ya Dusit D2 kuandaliwa leo

Ibada ya misa ya wafu kwa ajili ya wafanyikazi 6 wa hoteli ya Dusit D2 waliouwawa kwenye shambulizi la kigaidi wiki jana inaandaliwa leo. Usimamizi wa hoteli hiyo umesema maandalizi yamekamilika kwa ajili ya ibada hiyo katika kanisa la Consolata Shrine mtaani Westlands. wafanyikazi wa hoteli hiyo waliouwawa ni Beatrice Mutua, Bernadette Konjaio, Erickson Mogaka, Trufosa Nyaboke, Dedricks Lemisi,  na Zachary Nyabwaga. Ibada hii itaandaliwa siku moja baada ya ile ya wafanyikazi 6 kampuni ya Cellulant waliouwawa kwenye shambulio hilo kuandaliwa jana.

Show More

Related Articles