HabariMilele FmSwahili

Shughuli za kawaida zarejelea Dusit D2 eneo la 14 Riverside

Shughuli za kawaida zimerejelewa Dusit D2, eneo la 14 Riverside walioacha magari na bidhaa zingine za afisi katika ene hilo wakiruhusiwa kuchukua mali zao leo. Usalama umedumishwa, vikosi vya usalama vikiwakagua kwa kikamilifu wanaofika kukusanya bidhaa zao. Miongoni mwa taratibu zilizowekwa ni lazima uwe umesajili gari unaloendesha, pale ulipokuwa umeligesha, rangi yake na aina ya gari pamoja na nambari yake ya usajili kabla ya kuruhusiwa kulichukua.

Anasema licha ya taratibu hizi wameridhishwa na jinsi vikosi vya usalma vinashughulikia hali hii ingawa hayuko tayari kurejea kazini wakati wowote kutoka sasa.

Show More

Related Articles