Mediamax Network Limited

Jamaa mmoja akamatwa kwa tuhuma za kuwauwa wanawe wa miaka 10 na 3,Shauri Moyo Nairobi

Polisi kituo cha Buruburu hapa Nairobi wanamzuilia jamaa mmoja kwa tuhuma za kuwauwa wanawe wa miaka kumi na tatu mtawalia. Jamaa huyo mkaazi wa Shauri Moyo anatuhumiwa kuwapa sumu wanawe mnamo Jumapili kufuaita mzozo baina yake na mkewe. Watoto hao hawakuonekana tangu hiyo Jumapili suala ambalo lilwaelekea majirani kuvuna mlango na kuwapata wakiwa wamefariki. Mkewe ambaye alikuwa ameenda nyumbani huko magharibi baada ya mzozo amerejea leo kupatwa na taarifa hizo.