HabariMilele FmSwahili

Ibaada ya wafu ya wafanyikazi 6 wa Cellulant waliofariki katika shambulizi la Dusit D2 kuandaliwa leo

Ibaada ya wafu  ya watu 6 waliofariki katika shambulizi la hoteli ya Dusit D2 Jumanne wiki jana itaandaliwa katika kanisa la CITAM, iliyoko Valley Road hapa Nairobi, kuanzia saa nne asubuhi. Sita hao walikuwa wafanyikazi wa Cellulant. Miongoni mwa wanaotarajiwa kuhudhuria misa hiyo ni waziri wa habari na mawasiliano Joe Mucheru.

Haya yanajiri wakati eneO la 14Rriverside likifungulwia asubuhi ya leo kwa wenyeji wa eneo hilo.Aidha walioacha magari yao kwenye eneo la mkasa wa Dusit D2 pia wataruhusiwa kuyachukua leo bada ya kukamilika uchunguzi uliokuwa ukiendeshwa.

Show More

Related Articles