HabariMilele FmSwahili

Mahakama ya juu yaidhinisha ushindi wa seneta wa Lamu Anwar Loitiptip

Mahakama ya juu imeidhinisha ushindi wa seneta wa Lamu Anwar Loitiptip. Mahakama hiyo imebatilisha uamuzi wa mahakama ya rufaa mjini Mombasa uliotolewa Julai mwaka jana ambayo pia iliagiza tume ya uchaguzi IEBC kuandaa uchaguzi mpya wa useneta kauntu ya Lamu. Mahakama ya juu pia imetupilia mbali kesi za kupinga ushindi wa mbunge wa Gatundu Kaskazini Annie Wanjiku Kibe na Kangogo Bowen wa Marakwet Mashariki. Hata hivyo mbunge wa Wajir Mashariki Ahmed Kolosh amepoteza kiti chake. Mahakama hiyo imeagiza uchaguzi kuandaliwa upya eneo hilo ikisema upigaji kura katika kituo cha qara ulikumbwa na hitilafu.

Show More

Related Articles