HabariPilipili FmPilipili FM News

Mahakama Ya Juu Yaidhinisha Ushindi Wa Seneta Loitiptip

Mahakama ya juu hatimaye imeidhinisha ushindi wa seneta wa Lamu Anwar Loitiptip.

Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa na mpinzani wake Hassan Albeity.

Awali mahakama ya rufaa ilibatilisha ushindi wa Seneta Loitiptip  kwa msingi kuwa uchaguzi uliingia dosari.

Aidha kabla ya hapo mahakama kuu ya Malindi ilikuwa imetupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wake kwenye uchaguzi wa agosti 8 mwaka wa 2017 kwa msingi kuwa LoitipTip alichaguliwa kihalali.

Show More

Related Articles