HabariPilipili FmPilipili FM News

Mombasa Isalama Asema Kamishna Achoki.

Kamishna wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki amewahakikishia usalama wakaazi na wageni wanaozuru mji wa Mombasa.

Hakikisho lake linajiri siku chache baada ya shambulizi la kigaidi kufanyika kwenye hoteli ya DUSIT D2 jijini Nairobi.

Achoki amewashauri wakaazi kutokuwa na wasiwasi akisema serikali inafanya kazi na vitengo vyote vya usalama kuhakikisha usalama wa mwananchi.

Amewahimiza wakaazi wa Mombasa kuripoti visa vyote vinavyotishia usalama wa mwananchi.

Show More

Related Articles