HabariMilele FmSwahili

Mahakama ya Leba yatoa muda zaidi kwa mchakato wa upatanisho baina ya KNUT na TSC

Yakijiri hayo mahakama ya Leba imetoa muda wa majuma mawili zaidi kwa mchakato wa kupata mwafaka baina ya walimu na tume ya kuwaajiri TSC. Mahakama hiyo imeiagiza kamati ya upatanisho wa pande hizo mbili  kuwasilisha ripoti yake ifikiapo Januari 31. Mahakama hiyo pia imewaagiza wawakilishi wa knut na TSC kuafikiana kuhusu tarehe mpya ya kuandaa mazungumzo kuhusiana na lalama za walimu. kati ya mengine muungano wa knut umekuwa ukitaka TSC kutekelea masuala manne ikiwemo kuwapandisha walimu madaraka.

Show More

Related Articles