HabariMilele FmSwahili

Waziri Amina na Belio Kipsang kuhojiwa na wabunge kuhusu utata wa mtaala mpya wa elimu

Waziri wa elimu balozi Amina Mohammed na katibu wake Belio Kipsang wanatarajiwa leo kufika mbele ya kamati ya bunge la taifa kuhusu elimu kutoa maeleo zaidi kuhusu utekelezwaji wa mtaala mpya wa 2-6-6-3. Mkao huu unafuata kile ambacho kimetajwa kama mkanganyiko uliokuwepo hapo nyuma kuhusu utejkelezaji wa mtaala huo baada ya Amina kusema utahairishwa hadi mwaka wa 2020 kabla ya kubadili na msimamo nwa kusema utatekelezwa kuanzia mwaka huu.

Aidha kamait hiyo inayoongozwa naye mbunge wa Tinderet Julius Melly itakuwa inadurusu masuala yanayohusiana na sheria ya utekelezwaji mfumo huo. Wabugne wanatarajiwa kupitisha sheria hiyo wakirejelea vikao Februari.

Show More

Related Articles